Dominika ya 23 Mwaka B
DOMINIKA YA 23 MWAKA B WA KANISA
TAREHE 09/09/2018
TAREHE 09/09/2018
MICHANGO DOMINIKA ILIYOPITA TAREHE 02/09/2018
PAROKIANI
Sadaka Wanaume Sh. 335,200
Sadaka Wanawake Sh. 417,450
Shukrani Wanaume Sh. 170,600
Shukrani Wanawake Sh. 176,450
Jumla Wanaume Sh 505,800
Jumla Wanawake Sh 593,900
Jumla Kuu Sh. 1,099700
Sadaka ya wiki Sh. 54,250
Boksi la Ujenzi Sh. 22,650
Asanteni sana kwa ukarimu wenu, Mungu
awabariki.
MATANGAZO YA NDOA
TANGAZO LA KWANZA
Charles Evodi Mathias na Rehema Joachim Pascal wote
wa Jumuiya ya Mt. Karoli Lwanga
TANGAZO LA PILI
Yohana Andrea Makuo anatarajia kufunga ndoa na Flora
Michael Simon, wote wa kutoka Jumuiya ya Mt. Elizabeth
TANGAZO LA TATU
Edward Elias Diwani wa Jumuiya ya Utatu Mtakatifu na
Maria Magdalena Rogath Joseph Kiria wa Jumuiya ya Familia Takatifu Parokia ya Ukonga
USAFI NA HUDUMA KANISANI
Tunawashukuru JUMUIYA YA MT.
MARIA MAGDALENA walio
tusaidia kufanya usafi ndani na nje
pamoja na kutoa huduma kwa wiki nzima Kanisani, Kwa wiki inayoanza tunaomba JUMUIYA
YA MT. PHILIPO watusaidie.
Pia JUMUIYA YA MT. YOHANE PAULO WA PILI wajiandae.
IBADA ZA JUMA HILI.
ALHAMISI : Kumbukumbu
ya Mtakatifu Yohane Krisostomi, Askofu na Mwalimu wa Kanisa. Pia Ibada ya
kuabudu saa 11:00 jioni kama kawaida, Kwaya ya Mt. Theresia na Wawata
watusaidie
IJUMAA : Sikukuu
ya Kutukuka kwa Msalaba, Misa ya jioni kama kawaida
JUMAMOSI : Kumbukumbu
ya Bikira Maria wa Mateso
DOMINIKA IJAYO NI DOMINIKA YA 24 MWAKA B WA KANISA
TAREHE 16/09/2018
MENGINEYO
1.
Matangazo
ya UWAKA
i.
Viongozi
wote wa Uwaka kila Jumuiya kuanzia leo mnaombwa kuwasilisha mchango wa shilingi
50,000 kwa ajili ya Dada wadogo tarehe 14/10/2018. Safari hii, badala ya
Mbagala, tutakwenda katika kituo chao kingine huko Visiga. Hivyo mchango huo
uanze mapema.
ii.
Viongozi
wa Uwaka wa kila Jumuiya jumapili ijayo tarehe 16 mnaombwa kuhudhuria kikao cha
dharura mara bada ya Misa ya kwanza. Kuna jambo la muhimu sana.
2.
Uongozi
wa WAWATA unawakumbusha jumuiya mbazo hawajamaliza michango wajitahidi kutoa
michango wanayodaiwa nda Dekania. Jumuiya zifuatazo hawajato hata senti tano,
ambazo ni Maria Goreth, Kristo Mfalme, Mt. Anna na Mt. Benedict.
3.
Kutakuwa
na tamasha la Kwaya litakalofanyika tarehe 23/09/2018 hapa Parokiani. Tunawakumbusha
viongozi wa Jumuiya kuwasilisha fedha za kuponi za tamasha la Kwaya. Kila
Jumuiya inaombwa kuwasilisha shilingi 16,000. Ziletwe ofisi ya Parokia
4.
Karismatiki
Katoliki Parokia ya Vingunguti wanawatangazia waamini wote kuwa Mkutano wa wiki
ya Neema, ulioanza tarehe 07/09/2018 unaendelea hadi tarehe 16/09/2018 katika
viwanja vya Parokia ya Vingunguti. Muda ni saa 9:00 Mchana, Wote mnakaribishwa.
5.
Sikukuu
ya Komunyo ya kwanza itafanyika tarehe 7/10/2018. Watoto watakaofaulu mitihani
watapokea. Pia mkutano wa Wazazi wa watoto wa Komunyo ya kwanza kwa wanaofanya
mafundisho ni siku ya Jumamosi tarehe 15/09/2018 saa 9:00 Alasiri katika ukumbi
wa Parokia.
6. Kanda No 7,8 na 9, watasali pamoja
tarehe 15/09/2018.
7. Kutakuwa na Misa ya maadhimisho ya
Jubilei ya Miaka 150 kwenye kanda no 7,8 na 9. Misa itafanyika Jumamosi ijayo saa
12:15 alfajiri maeneo ya Matofalini kwa perapera. Viongozi wafike Parokiani
kuwachukua mapadre. Pia kanda No 10, 11, na 12 watasali pamoja tarehe
22/09/2018. Viongozi walete taarifa mapema kuhusu mahali itakapofanyikia. Pia unawakumbusha
viongozi wa kila kanda kuja na Tsh 50,000/= ya matendo ya huruma
8.
Kilele
cha Saidia Jimbo Kiparokia kitakuwa Mwezi wa 10, hivyo tunaomba viongozi wa Jumuiya
waanze kuwasilisha michango ofisini kwa baba Paroko
9.
Tunaendelea
kuwakumbusha waamini kuwa tunapotoka nje tukumbuke kuweka chochote kwenye
sanduku la ujenzi.
10.Jumapili ya terehe 16/09/2018,
kutakuwa na Ibada ya kuwaaga viongozi waliohama kwenye umeoja wtu wa Makanisa.
Ibada itafanyika katika Kanisa la KKKT saa tisa mchana . Mnakaribishwa sana.
11.Kamati ya uhamasishaji mnaombwa
kuonana na viongozi wa Kamati Tendaji ya Parokia. Wakutane kwenye ofisi ya
Parokia baada ya Misa ya Kwanza.
Comments
Post a Comment