Dominika ya 22 Mwaka B
DOMINIKA YA 22 MWAKA B WA KANISA
TAREHE 02/09/2018
TAREHE 02/09/2018
MICHANGO DOMINIKA ILIYOPITA TAREHE 26/08/2018
PAROKIANI
Sadaka Wanaume Sh. 344,600
Sadaka Wanawake Sh. 322,300
Shukrani Wanaume Sh. 115,750
Shukrani Wanawake Sh. 100,800
Jumla Wanaume Sh 460,350
Jumla Wanawake Sh 423,100
Jumla Kuu Sh. 883,450
Sadaka ya wiki Sh. 87,850
Boksi la Ujenzi Sh. 21,200
Pia shukrani kwa Jumuiya ya Mt Yuda Thadei kwa bahasha
ya Ujenzi 100,000
Asanteni sana kwa ukarimu wenu, Mungu
awabariki.
MATANGAZO YA NDOA
TANGAZO LA KWANZA
Yohana Andrea Makuo anatarajia kufunga ndoa na Flora
Michael Simon, wote wa kutoka Jumuiya ya Mt. Elizabeth
TANGAZO LA PILI
Edward Elias Diwani wa Jumuiya ya Utatu Mtakatifu na
Maria Magdalena Rogath Joseph Kiria wa Jumuiya ya Familia Takatifu Parokia ya Ukonga
TANGAZO LA TATU
Menas Gervas Kalelwa
anatarajia kufunga ndoa na Lidia Jofrey Kanyoka wote kutoka jumuiya ya Mt.
Kolleta
USAFI NA HUDUMA KANISANI
Tunawashukuru JUMUIYA YA MT.
YUDA THADEI walio
tusaidia kufanya usafi ndani na nje
pamoja na kutoa huduma kwa wiki nzima Kanisani, Kwa wiki inayoanza tunaomba JUMUIYA
YA MT. MARIA MAGDALENA watusaidie. Pia JUMUIYA YA ---------------------- wajiandae.
IBADA ZA JUMA HILI.
JUMATATU : Kumbukumbu
ya Mtakatifu Gregori Mkuu, Papa na Mwalimu wa Kanisa
ALHAMISI : Ibada
ya kuabudu saa 11:00 jioni kama kawaida
IJUMAA : Misa
ya jioni saa 11:00 kama kawaida.
JUMAMOSI : Sikukuu
ya kuzaliwa Bikira Maria
DOMINIKA IJAYO NI DOMINIKA YA 23 MWAKA B WA KANISA
TAREHE 09/09/2018
MENGINEYO
1.
Matangazo
ya UWAKA
i.
Kamati
tendaji ya Uwaka Parokia inawashukuru Wanaume wote waliojitokeza na kushiriki
semina Jumapili iliyopita. Asanteni sana.
ii.
Wanaume
wa Kanda No 1 na 2 leo watakutana katika Jumuiya ya Mt. Joseph Mfanyakazi
nyumbani kwa Ndugu Francis Miso (Baba Tungu) saa 10 kamili jioni
iii.
Viongozi
wote wa Uwaka kila Jumuiya kuanzia leo mnaombwa kuwasilisha mchango wa shilingi
50,000 kwa ajili ya Dada wadogo tarehe 14/10/2018. Safari hii, badala ya
Mbagala, tutakwenda katika kituo chao kingine huko Visiga. Hivyo mchango huo
uanze mapema.
2.
Uongozi
wa Wawata wanawataarifu viongozi wote watano wa kila Jumuiya kuwa leo kutakuwa
na kikao parokiani baada ya Misa ya kwanza. Kwa zile Jumuiya ambazo bado
hazijamaliza madeni yao wafike na michango hiyo. Ni kikao muhimu sana.
3.
Leo
baadaya Misa ya pili, kutakuwa na kikao cha dharura cha vijana (VIWAWA),
wahusika ni viongozi wa Vijana (Watano) wa kila Jumuiya Parokiani na Kigangoni.
4.
Wamisionari
wadogo wa Cottolengo wameanza kutoa huduma ya kuuza vipeperushi vya masomo ya
Jumapili, kwa bei ya shilingi 200 tu.
5.
Karismatiki
Katoliki Parokia ya Vingunguti wanawatangazia waamini wote kuwa kutakuwa na
Mkutano wa wiki ya neema, utakaoanza tarehe 07/09/2018 – 16/09/2018 katika
viwanja vya Parokia ya Vingunguti. Wote mnakaribishwa.
6.
Kutakuwa
na tamasha la Kwaya litakalofanyika tarehe 23/09/2018 hapa Parokiani. Tiketi au
kuponi kwa ajili ya kushuhudia tamasha ni shilingi 3,000 na 5,000
7.
Sikukuu
ya Komunyo ya kwanza itafanyika tarehe 7/10/2018. Watoto watakaofaulu mitihani
watapokea. Siku ya mtihani wa Komunyo ya kwanza ni siku ya Jumatano saa 4:00
Asubuhi. Pia mkutano wa Wazazi wa watoto
wa Komunyo ya kwanza kwa wanaofanya mafundisho ni siku ya Jumamosi tarehe
15/09/2018 saa 9:00 Alasiri katika ukumbi wa Parokia.
8. Jumamosi tarehe 08/09/2018, kutakuwa
na Misa ya Maadhimisho ya Misa ya Jubilei ya miaka 150 ya uinjilishaji katika
Kanda No 5 na NO 6, itakayofanyikia nyumbani kwa Ndugu Gustav Banzi – Jumuiya
ya Mt Timoteo saa 12:15 alfajiri. Kanda yenye zamu waje Parokiani kuwachukua
Mapadre.
9. Kanda No 7,8 na 9, watasali pamoja
tarehe 15/09/2018. Viongozi walete taarifa mapema kuhusu mahali
itakapofanyikia.
Pia kanda No 10, 11, na 12 watasali pamoja tarehe 22/09/2018.
Pia kanda No 10, 11, na 12 watasali pamoja tarehe 22/09/2018.
10.Kutakuwa na matendo ya huruma
Kiparokia tunapoelekea kilele cha maadhimisho ya Jubilei ya miaka 150, hivyo
kila kanda inaombwa kuchangia shilingi 50,000 kutoka kwenye mfuko wa Kanda.
Pesa hiyo itakabidhiwa wakti wa Ibada zinazoendelea kwenye kanda.
11.Kilele cha Saidia Jimbo Kiparokia
kitakuwa Mwezi wa 10, hivyo tunaomba viongozi wa Jumuiya waanze kuwasilisha
michango ofisini kwa baba Paroko
12.Jumatatu ijayo Kamati tendaji ya
Parokia inaomba kukutana na kamati ya uhamasishaji. Kikao kitafanyika hapa
Parokiani saa 11:00 jioni. Mnaombwa kuhudhuria bila kukosa. Ni muhimu sana.
Comments
Post a Comment